IQNA

Warsha ya utafiti wa Kiislamu kufanyika Wales

13:20 - December 09, 2010
Habari ID: 2045033
Warsha ya utafiti wa masuala ya Kiislamu imepangwa kufanyika tarehe 9 Machi mwakani katika Chuo Kikuu cha Wales.
Kituo cha upashaji habari cha Heacademy kimetangaza kuwa warsha hiyo itasimamiwa na kanali iliyoasisiwa hivi karibuni ya utafiti wa Kiislamu ya Uingereza kwa ajili ya walimu wa masuala ya utafiti wa Kiislamu katika jumuiya ya elimu ya juu ya Wales.
Lengo la warsha hiyo limetajwa kuwa ni kuwakutanisha pamoja walimu wa masuala ya utafiti wa Kiislamu katika nyanja mbalimbali za teolojia, historia, siasa, fasihi, elimu jamii, anthropolojia, sheria, biashara na masoko.
Washiriki katika warsha hiyo watapata fursa ya kusoma na kuchunguza mbinu za kufundisha elimu za Kiislamu huko Wales. 709347
captcha