IQNA

Harakati inayopinga ubaguzi Ufaransa yapinga mkutano dhidi ya Uislamu

18:40 - December 13, 2010
Habari ID: 2047530
Harakati ya Kukabiliana na Ubaguzi na Kuimarisha Urafiki kati ya Watu ya Ufaransa (Mrap) imemtumia barua ya wazi Meya wa Paris ikilaani mpango wa kufanyika mkutano wa kimataifa wa kupiga vita Uislamu na Waislamu.
Katika barua hiyo harakati ya Mrap imeelezea wasiwasi wake kuhusu uamuzi wa makundi ya kibaguzi wa kuitisha mkutano wa kupiga vita Uislamu katika ngazi ya kimataifa mjini Paris utakaohudhuriwa na makundi na watu wenye mitazamo ya kibaguzi kutoka maeneo mbalimbali duniani. Harakati hiyo imetoa wito wa kufutiliwa mbali mkutano huo.
Sehemu moja ya barua hiyo ya wazi kwa Meya wa Paris imesema kuwa watayarishaji wa mkutano huo ni watu wanaojulikana vyema katika jamii ya Ufaransa kwa harakati zao za kibaguzi na kuchochea fikra za wananchi. Imesisitiza kuwa makundi hayo yanawahamasisha vijana kufanya ghasia na kutekeleza ubaguzi kwa jina la kulinda utambulisho wa kitaifa.
Harakati ya kupinga ubaguzi nchini Ufaransa imemtaka Meya wa Paris kufanya mazungumzo na viongozi husika kwa ajili ya kuzuia mkutano huo unaopiga vita Uislamu katika mji mkuu wa Ufaransa. 711708
captcha