IQNA

Kibali cha kuwekwa mabango na vitambaa vya maomboleza ya Muharram Pakistan

15:56 - December 14, 2010
Habari ID: 2047718
Viongozi wa Pakistan wametoa kibali cha kuwekwa mabango na vitambaa vinavyotangaza maombolezo ya kuuawa shahidi Imam Hussein (as) katika mji wa Lahore nchini humo.
Gazeti la Tribune, limeandika kuwa kwa mujibu wa kibali hicho Waislamu wa madhehebu ya Shia wamepewa fursa ya kuweka mabango na vitambaa vilivyo na maandishi ya maombolezo ya Imam Hussein (as) na mapambano yake dhidi ya watawala madhalimu katika ardhi ya Karbala, kwenye majengo na mitaa yote ya mji huo.
Akizungumzia suala hilo, Shir Shah mmoja wa wanachama wa jumuiya ya Kishia ya Pakistan amesema kuwa Mashia na Masuni ni ndugu na kwamba lengo la kuwekwa mabango na vitambaa hivyo ni kuimarisha mwamko wa umma kuhusiana na mwezi mtukufu wa Muharram na mapambano ya Imam Hussein (as).
Amesema matangazo na maandishi yaliyoandikwa kwenye mabango na vitambaa hivyo kamwe hayadharau wala kukosea heshima imani na itikadi za madhehebu mengine ya Kiislamu bali kinyume chake, yanahubiri umoja na kuvumiliana miongoni mwa wafuasi wa madhehebu tofauti ya Kiislamu. 712082
captcha