Kituo cha habari cha NEWSOK kimeripoti kuwa Kituo cha Kiislamu cha Msikiti wa Oklahoma City kimeanza kutekeleza mpango huo adhuhuri ya leo Jumamosi.
Mpango huo wa kuwapa chakula watu wasiokuwa na makazi katika sikukuu za Krismasi unatekelezwa kwa ushirikiano wa Baraza la Kiislamu la Oklahoma City na Baraza la Uhusiano wa Kiislamu na Marekani tawi la Oklahoma.
Mwenyekiti wa Kituo cha Kiislamu cha Oklahoma Imad Anchasi amesema kuwa dini ya Kiislamu inatufunza kuwasaidia watu wasiojiweza.
Msemaji wa kituo hicho Saad Muhammad pia amesema, kwa mujibu wa mpango huo, watu wasiojiweza wametayarishiwa usafiri wa kuwapeleka katika msikiti wa mji huo, na mbali na chakula watapewa zawadi ya blanketi.
Amesema kuwa sikukuu ya Krismasi ni wakati muafaka wa kutoa chakula kwa watu wasioweza kumudu gharama za maisha yao. 717449