IQNA

Kikao cha 20 cha Taasisi ya Fiqhi ya Kiislamu chaanza Makka

16:40 - December 25, 2010
Habari ID: 2052980
Kikao cha 20 cha Taasisi ya Fiqhi ya Kiislamu kimeanza leo tarehe 25 Disemba katika sekretarieti ya Jumuiya ya Kimataifa ya Uislamu mjini Makka Saudi Arabia.
Kikao hicho ambacho kitaendelea na kazi zake hadi tarehe 30 Disemba kinahudhuriwa na zaidi ya wanafikra 60 wa Kiislamu na wataalamu kadhaa ma masuala ya fiqhi na sheria za Kiislamu.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ulimwengu wa Kiislamu Abdullah bin Abdulmuhsin al Turki amesema kuwa tafiti na makala 35 za kifiqhi kuhusu masuala ya dunia ya sasa, matatizo yaliyojitokeza katika zama hizi na masuala ya kiuchumi, kisiasa na kitiba ya maisha ya Waislamu yatawasilishwa katika kikao hicho.
Ameongeza kuwa maudhui nyingine za kikao hicho cha Makka ni kuchunguza masoko ya fedha, uendeshaji wa masuala ya benki za Kiislamu na jinsi ya kuchukua maamuzi ya kidini katika nyanja hizo. 717634

captcha