IQNA

Khutba ya Sala ya Ijumaa Tehran

12:07 - January 01, 2011
Habari ID: 2056229
Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran Hujjatul Islam Sayyid Ahmad Khatami amesema: “Aina mbaya zaidi ya kuzusha mfarakano ni kuzusha mfarakano baina ya wananchi na mfumo wa Kiislamu jambo ambalo maadui wa kigeni wameshindwa kufanya.
Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran ameongeza kuwa tarehe 30 Desemba ni siku ya hamasa kubwa kwa taifa la Iran na kwamba ni siku ya kubai utawala wa faqihi.
Akihutubia halaiki kubwa ya waumini katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Tehran, Sayyed Ahmad Khatami ameashiria umuhimu wa kushiriki kwa wingi taifa la Iran katika hamasa ya tarehe 30 Desemba mwaka jana katika kuhami Utawala wa Faqihi. Amesema siku hiyo ilikuwa siku ya kujiweka mbali taifa la Iran na maadui. Ameitaja siku hiyo kuwa siku iliyojaa fahari katika historia ya mapinduzi ya Kiislamu.
Khatibu wa Sala ya Ijumaa amelinganisha matukio ya mwaka jana ya Iran na fitina zilizoukabili utawala wa Imam Ali AS mwanzoni mwa Uislamu. Ayatullah Khatami ameashiri mbinumbali mbali zilizokuwa zikitumiwa na wenye kuzusha fitina na kuzitaja kuwa ni pamoja na kueneza uongo na tuhuma zisizo na msingi, kueneza wasi wasi, kuvunjia heshima matukufu ya kidini, kueneza propaganda za vyombo vya habari, kutumia vibaya matukufu hasa jina la Imam Khomeini MA na kuibua mifarakano hasa baina ya wananchi na mfumo wa Kiislamu. Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Ayatullah Khatami ameashiria matukio ya kigaidi katika mipaka ya mashariki mwa Iran na magaidi walio na makao yao katika ardhi ya Pakistan. Ametoa wito kwa serikali ya Pakistan kuwatia mbaroni magaidi hao na kuwakabidhi kwa Iran haraka iwezekanavyo.
Ayatullah Khatamu amegusia hatua ya kupitishwa sheria ya kupiga marufuku Hijabu katika shule za Jamhuri ya Azerbaijan na kutoa wito kwa serikali ya nchi hiyo kuacha kuwashinikiza Waislamu hasa Mashia waliowengi nchini humo.
721439

captcha