IQNA

Sheikh Hassan Saffar akosoa vikali hatua ya kufukuzwa mwalimu Shia Saudia

14:38 - January 02, 2011
Habari ID: 2057391
Msomi na mwanafikra wa Kiislamu wa madhehebu ya Shia wa Saudi Arabia Sheikh Hassan Saffar amekosoa hatua ya serikali ya nchi hiyo ya kumfukuza kazi mwalimu Shia kwa sababu tu ya kufundisha ibada ya swala kwa mujibu wa madhehebu ya Shia na kusalisha swala ya jamaa shuleni.
Hujjatul Islam Hassan Saffar ambaye pia ni imamu wa swala ya Ijumaa ya mji wa Qatif mashariki mwa Saudi Arabia amesema inastaajabisha mno kuona Wizara ya Elimu ya Saudi Arabia ikimfukuza mwalimu kwa sababu tu ya kufundisha wanafunzi ibada ya swala kwa mujibu wa madhehebu yao ya Shia.
Sheikh Saffar ameitaka wizara hiyo itazame upya amuzi wake na kuheshimu haki za binadamu.
Amesema inasikitisha kwamba baadhi ya makundi yenye misimamo mikali inafanya jitihada za kulazimisha mitazamo yao kwa watu wote wa jamii na kupuuza mitazamo ya madhehebu nyingine. Amesema makundi hayo yanatambua mitazamo ya madhehebu nyingine za Kiislamu kuwa ni kosa la jinai.
Sheikh Hassan Saffar amesisitiza kuwa wanafunzi wanapaswa kufunzwa mambo mbalimbali kwa mujibu wa madhehebu yao na kwamba mafunzo yanayotolewa kwa wanafunzi wa kila eneo yanapaswa kufuata madhehebu ya wakazi wa eneo hilo.
Ni vyema kukumbusha hapa kuwa Wizara ya Elimu ya Saudi Arabia wiki iliyopita ilimfuta kazi Fauzi Shanar kwa kosa la kuwafundisha swala wanaunzi wa Kishia kwa mujibu wa madhehebu yao. Kosa jingine la mwalimu huyo lilikuwa kusalisha swala ya jamaa shuleni hapo. 722660
captcha