IQNA

Msafara wa Asia NO-1 wawasili Gaza

16:43 - January 03, 2011
Habari ID: 2058242
Msafara wa misaada ya kibinadamu wa Asia NO-1 umewasili katika Ukanda wa Gaza mapema leo kupitia kivuko cha Rafah nchini Misri.
Shirika la habari la Kuwait limeripoti kuwa misaada ya msafara huo ambayo ina uzito wa zaidi ya tani 100 za bidhaa za kitiba, kiafya, maziwa ya watoto wadogo na vifaa vinavyotumiwa na watu wenye ulemavu uliotokana na mashambulizi ya Israel dhidi ya raia wa eneo hilo inatazamiwa pia kuwasili leo katika eneo la Gaza.
Msafara huo unajumuisha wanaharakati zaidi ya mia moja wa nchi mbalimbali za Asia na watetezi wa haki za binadamu kutoka maeneo mbalimbali duniani.
Msafara huo umepokewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Serikali ya Kuvunja Mzingiro wa Gaza Ahmad Yusuf, shakhsia na viongizi wengine wa eneo hilo.
Ahmad Yusuf amewashukuru viongozi wa nchi zilizofanikisha safari ya msafara huo akisisitiza juu ya mchango mkubwa wa misafara kama hiyo katika kuvunja mzingiro haramu wa utawala wa Kizayuni dhidi ya raia milioni moja na nusu wa Ukanda wa Gaza.
Msafara wa Asia NO-1 wa misaada ya kibinadamu kwa ajili ya Gaza unajumuisha pia wahadhiri wa vyuo vikuu, waandishi habari, wanasheria na wanaharakati wa jumuiya za kiraia wa dini mbalimbali. 723466
captcha