Nara ya marasimu hayo ilikuwa; 'Uislamu ni dini ya udugu na wepesi, sio mabavu na ugaidi.' Akizungumza katika marasimu hayo, Nassir Saidi, mkuu wa ofisi ya Shahidi Sadr amesema kuwa kuna baadhi ya makundi ya kigaidi na yanayotumia mabavu yaliyo na lengo la kuwagawa wananchi wa Iraq katika misingi ya kimadhehebu jambo ambalo ametahadharisha kuwa litakuwa na athari mbaya na hatari kubwa ya ksiaisa, kiuchumi na kijamii kwa nchi hiyo.
Katika upande wa pili, Quswei as-Suheil, Naibu Spika wa Bunge la Iraq aliyehudhuria pia marasimu hayo amesema kuwa kulengwa kwa haram tukufu ya Askariyein (as) kwa hakika ni kulengwa kwa thamani za Kiislamu.
Kwa upande wake, Ahmad al-Husna, mwakilishi wa Wakfu za Kisuni nchini Iraq alisema katika marasimu hayo kwamba kuna udharura wa kuimarishwa umoja na mshikamano wa wananchi wote wa Iraq na kusimama imara dhidi ya mifarakano, hitilafu na ugaidi. 723490