Alexander Prokhanov mwandishi na mhariri mkuu wa jarida la kila wiki la Zavtra amayasema hayo wakati anakagua Kituo cha Uhakiki wa Kumputa wa Sayansi za Kiislamu katika mji mtakatifu wa Qum. Ameongeza kuwa: "Nimeshangazwa mno kona jinsi sayansi za Kiislamu zinavyoenezwa dunia nchini Iran hususan katika mji wa Qum kwa kutumia teknolojia na lugha ya kisasa."
Alexander Prokhanov ambaye ana shahada ya uzamivu katika masuala ya anga anasema: "Nilikuwa nikidhani kwamba nikiwa nchini Iran hususan katika mji wa Qum sitaona chochote isipokuwa misikiti na nembo za kidini na kamwe zikudhani kwamba ninaweza kushuhudia masuala ya kiteknolojia katika mji huu."
Prokhanov ambaye ameshangazwa mno na kituo cha sayansi na utafiti wa masuala ya kidini cha Qum ameongeza kuwa amefurahi mno kuona kwamba fikra zangu zote hazikuwa sahihi na kwamba hii leo kuna vituo vinavyoeneza itikadi na fikta za kidini kwa kutumia teknolojia ya kisasa.
Mhariri wa mkuu wa jarida la Zavtra la Russia ambaye yeye mwenyewe ni Mkristo wa madhehebu ya Kiprotestanti anasema: "Mtazamo wangu kuhusu Iran hususan mji wa kielimu wa Qum umebadilika na kwamba mji huo una historia ndefu ya utafiti, uchunguzi na sayansi ya Kiislamu. 724313