IQNA

Ayatullah Sistani, nguzo muhimu ya umoja nchini Iraq

13:31 - January 08, 2011
Habari ID: 2060457
Akizungumza mara baada ya kuonana na kuzungumza na Ayatullahil Udhma Ali Sistani katika mji mtakatifu wa Najaf, Ali Akbar Swalehi, msimamizi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kwamba kiongozi huyo wa kidini ni nguzo muhimu ya umoja kati ya makundi yote ya Iraq.
Swalehi amesema amekuwa na mazungumzo muhimu na yaliyofana sana na kiongozi huyo wa kidini. Amesema alikuwa amebeba ujumbe wa wanazuoni wa Qum kwa marja' huyo muhimu wa Najaf na kuelezea matumaini yake kwamba juhudi kubwa anazofanya mwanazuoni huyo mashuhuri zitaimarisha umoja, uthabiti na utulivu wa kudumu nchini Iraq.
Swalehi aliwatembelea mamarja' wengine pia katika mji huo mtakatifu.
Alielekea nchini Iraq siku ya Jumatano kwa lengo la kuwapongeza Wairaqi kwa kubuniwa serikali mpya ya nchi hiyo pamoja na kufanya mazungumzo na viongozi wa serikali hiyo. 725671
captcha