IQNA

Wanachuo Waislamu kutoka nchi 45 watembelea kituo cha Nour

14:06 - January 08, 2011
Habari ID: 2060747
Mkurugenzi wa Masuala ya Kimataifa wa Kituo cha Uhakiki wa Komputa wa Sayansi za Kiislamu cha Nour amesema kuwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Jamiatul Mustafa al Alamiyya kutoka nchi 45 wametembelea kituo hicho na kukagua shughuli mbalimbali zinazofanyika hapo.
Muhsin Meschi Mkurugenzi wa Masuala ya Kimataifa wa Kituo cha Uhakiki wa Komputa wa Sayansi za Kiislamu cha Nour katika mji mtakatifu wa Qum amesema viongozi na baadhi ya maafisa wa Chuo Kikuu cha al Mustafa al Alamiyya walifuatana na wanachuo hao. Ameongeza kuwa wanafunzi 54 wa chuo hicho walitembelea kituo cha Nour ikiwa ni sehemu ya mkutano wa kila mwaka wa wanafunzi wa kituo hicho cha taaluma na sayansi za Kiislamu. Amesisitiza kuwa katika mkusanyiko huo wanachuo huwasilisha mitazamo yao na kuzungumzia masuala na mahitaji ya kimataifa ili kuboresha masomo na huduma mpya za kimaanawi zinazotolewa kwa wanachuo hao.
Meschi amesema katika mkutano huo wa kila mwaka pande zote mbili hufanya jitihada za kutambua mahitaji ya dunia ya sasa ili kutayarisha uwanja mzuri wa kubuniwa mipango mipya ya kukidhi mahitaji hayo.
Amesema kuwa miongoni mwa malengo ya mkusanyiko huo ni kuimarisha upande wa kiroho na kimaanawi wa wanachuo hao, kupanua zaidi uwezo wao wa kielimu na kuwafahamisha mabadiliko yaliyotokea katika medani ya elimu na utafiti wa Kituo cha Uhakiki wa Kopyuta wa Sayansi na Maarifa ya ya Kiislamu.
Amesisitiza kuwa wanafunzi wa Jamiatul Mustafa al al Alamiyya kutoka mabara manne ya dunia wamehudhuria kikao hicho. Amesema wanachuo elfu 20 kutoka nchi 100 wanapata elimu katika Chuo Kikuu cha Jamiatul Mustafa al Alamiyya katika mji mtakatifu wa Qum, suala ambalo linakipa nafasi maalumu chuo hicho kati ya vyuo vingine vikuu vya kigeni. 726033
captcha