IQNA

Kongamano la 12 la Mafunzo ya Kiislamu kufanyika Illinois

13:59 - January 09, 2011
Habari ID: 2061432
Kongamano la 12 la Mafunzo ya Kiislamu litafanyika tarehe 22 hadi 24 Aprili katika jimbo la Illinois chini ya usimamizi wa Taasisi ya Kiislamu ya Kaskazini mwa Marekani (ISNA).
Mtandao wa Isna.net umeripoti kuwa kongamano hilo litafanyika chini ya anwani ya "maarifa, kuishi kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu" katika hoteli ya Westin O’Hare katika mji wa Rosemont jimboni Illinois.
Kongamano hilo la siku tatu litajadili maudhui mbalimbali kama Uislamu na mazingira, utumiaji wa mbinu mbalimbali za kifikra katika kufundisha elimu za Kiislamu, mbinu bora za kutalii na kuchunguza Uislamu na kadhalika.
Maudhui nyingine zitakazojadiliwa katika kongamano hilo ni kutathmini kazi za maafisa husika wa elimu, mafunzo ya lugha ya Kiarabu na kuratibu shughuli za shule za elimu za Kiislamu. 726942


captcha