Ratiba hiyo inasimamiwa na Jumuiya ya Wanafunzi Waislamu wa Chuo Kikuu cha British Columbia kwa lengo la kuzidisha maarifa ya jamii kuhusu Uislamu na Waislamu na kuondoa sura mbaya na isiyokuwa sahihi inayoenezwa kuhusu dini hiyo ya Mwenyezi Mungu.
Miongoni mwa ajenda za wiki hiyo ni kuonyesha filamu ya "Mjini Makka", "Muhammad, Mrithi wa Mitume", na hotuba kuhusu tauhidi na kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kufafanua itikadi na misingi ya Kiislamu. Vilevile kutafanyika vikao vya mijadala kuhusu itikadi za Kiislamu, Mitume na vitabu vitakatifu, mwanamke katika Uislamu, jihadi na kadhalika.
Chuo Kikuu cha British Columbia pia kitakuwa na kikao cha "Qur'ani:
Faslu ya Mwisho" ambacho kitachunguza mafundisho ya Qur'ani, misingi ya maadili iliyozungumziwa katika kitabu hucho na muujiza wa Qur'ani.
Maudhui nyingine itakayojadiliwa katika Wiki ya Ujue Uislamu ni Turathi ya Mtume Muhammad (saw) ambayo inalenga kuweka wazi nafasi ya mitume na sifa makhsusi za kiakhlaki za Mtume Muhammad (saw). 730533