IQNA

Warsha ya wanafunzi kutoka nchi 60 kufanyika kituo cha Nour

16:37 - January 17, 2011
Habari ID: 2066280
Wanafunzi wa zaidi ya nchi 60 wanatarajia kukutana katika kituo cha Nour kwa ajili ya warsha ya mafunzo ya kitaalamu ya jinsi ya kutumia programu za komputa za sayansi za Kiislamu na kibinadamu.
Warsha hiyo itafanyika kwa ushirikiano wa Chuo Kikuu cha al Mustafa al Alamiyyah na Kituo cha Uhakiki wa Kumputa cha Sayansi za Kiislamu.
Mkurugenzi wa kitengo cha masuala ya kimataifa wa Kituo cha Nour Muhsin Meschi ameliambia shirika la habari la IQNA kwamba warsha hiyo ambayo itawakutanisha pamoja wanafunzi zaidi ya 320 kutoka nchi 60 duniani ni ishara ya kuenea dini ya Uislamu na mafundisho ya dini hiyo na Ahlulbait wa Mtume (saw) duniani kote.
Muhsin Meschi ameongeza kuwa katika warsha hiyo kutaonyeshwa bidhaa mpya na jinsi ya kutumia teknolojia ya mawasiliano (IT) kwa ajili ya kutangaza dini ya Kiislamu na elimu ya Ahlulbait. Warsha hiyo itasimamiwa na wataalamu wa Kituo cha Uhakiki wa Kupyuta cha Sayansi za Kiislamu.
Amesema kuwa miaka miwili iliyopita kituo cha Nour kilipokea wasomi na wataalamu zaidi ya 1900 wa kigeni katika Kituo cha Uhakiki wa Kopyuta cha Sayansi za Kiislamu na kwamba hadi mwishoni mwa mwaka huu idadi hiyo itafikia 2500.
Warsha hiyo imepangwa kufanyika Jumatano ya wiki hii. 732285
captcha