IQNA

Kituo cha upashaji habari cha Islam kufunguliwa leo Saudia

10:27 - January 23, 2011
Habari ID: 2069004
Mtandao wa upashaji habari wa Islam utafunguliwa leo Jumapili nchini Saudi Arabia.
Mtandao huo unaosimamiwa na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Saudi Arabia utakuwa na habari kuhusu taaluma za Kiislamu na Qur'ani kwa lugha saba za Kiarabu, Kiingereza, Kifaransa, Kihindi, Kiholanzi, Kituruki, Malay na Kiindonesia.
Mtandao huo utakuwa na sehemu nne kuu ambazo ni Qur'ani, hadithi, turathi na hija na umra na kila sehemu itakuwa na mijadala kuhusu mauala mbalimbali na uchunguzi uliofanyika kuhusu somo husika.
Waziri wa Wakfu wa SaudiArabia Seikh Saleh bin Abdul Aziz Skeikh ndiye anayesimamia mtandao huo. 735090
captcha