IQNA

Ayatullah al Amri azikwa katika makaburi ya Baqii

17:43 - January 28, 2011
Habari ID: 2071356
Mwili wa mwanazuoni mashuhuri wa madhehebu ya Shia nchini Saudi Arabia Ayatullah Muhammad al Amri ulizikwa jana katika makaburi ya Baqii mjini Madina katika shughuli iliyohudhuriwa na maumini wengi waliokuwa na huzuni kubwa.
Maelfu ya Waislamu wa madhehebu ya Shia wa Saudi Arabia walisindikiza na kuzika mwili wa marehemu al Amri aliyefariki dunia Jumatatu iliyopita baada ya kusumbuliwa na ugonjwa kwa kipindi kirefu.
Maiti ya Ayatullah Muhammad Ali al Amri ilisaliwa sala ya maiti na maelfu ya Waislamu wa madhehebu ya Shia ambayo imeongozwa na Sayyid Ali Sayyid Nasir al Salman, mmoja kati ya wanazuoni mashuhuri wa Saudia.
Shughuli hiyo ya mazishi ilihudhuriwa na idadi kubwa ya maulamaa, wanazuoni na wanafikra wa mji mtakatifu wa Madina. Maulamaa na wanazuoni kutoka Iran, Lebanon, Kuwait na Bahrain pia wameshiriki katika mazishi hayo.
Ayatullah Muhammad Ali al Amri alikuwa akitambuliwa kuwa ndiye kiongozi wa kiroho wa Waislamu wa madhehebu ya Shia wa Saudi Arabia kutokana na nafasi yake ya juu ya kielimu na kiakhlaki. Nyumba ya mwanazuoni huyo daima ilikuwa ikijaa Waislamu wanaokwenda mjini Madina kuzuru kaburi tukufu la Mtume Muhammad (saw).
Ayatullah Muhammad Ali al Amri ambaye amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 90 alifungwa katika jela za utawala wa Saudi Arabia kwa kipindi cha miaka 45 kutokana na kufuata madhehbu ya Watu wa Nyumba ya Mtume Muhammad (saw). 737550
captcha