IQNA

Kikao cha Uislamu na Ushia kufanyika Uhispania

22:05 - January 29, 2011
Habari ID: 2072088
Kikao cha kielimu cha "Uislamu na Ushia nchini Uhispania, Zama za Sasa na Siku Zijazo" kimepangwa kufanyika Jumatatu ijayo mjini Tehran.
Kikao hicho ambacho kimetayarishwa na kundi la utafiti wa kiutamaduni wa ulimwengu wa Kiislamu la kituo cha mawasiliano ya kiutamaduni na kimataifa kitahutubiwa na Sayyid Ahmad Ridha Khadhari ambaye ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tehran.
Miongoni ma maudhui zitakazojadiliwa katika kikao hicho ni pamoja na 'kudhihiri Uislamu na madhehebu ya Shia nchini uhispania', 'hali ya sasa ya kiutamaduni na kijamii ya Waislamu wa Uhispania', 'ushirikiano wa kiutamaduni kati ya Uhispania na Iran na mustakbali wa ushirikiano huo'.
Wanafunzi wa vyuo vikuu, wahadhiri na wasomi wamealikwa kushiriki katika kikao hicho. 738141
captcha