Akizungumza na IQNA, Mbunge Ismail Kauthari amesema Majlisi inapaswa kuchukua hatua zaidi kuhakikisha kuwa mafundisho ya Qur'ani yanatekelezwa katika maisha ya kila siku nchini ili kujenga jamii bora.
Kauthari ametoa mapendekezo kadhaa kuhusu utekelezwaji kikamilifu mafundisho ya Qur'ani katika jamii ya Iran.
Akiashiria miongozo ya muasisi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Imam Khomeini MA, amesema chimbuko la fikra za Imam ni Qur'ani Tukufu na mafundisho ya Ahlul Bayt AS. Amesema jamii ya Iran inapaswa kuendelea kuzingatia fikra na miongozo ya Imam Khomeini.
Mbunge huyo amesema maadui wamekuwa wakijaribu kuidhuru Jamuri ya Kiislamu ya Iran kwa njia mbalimbali na kuongeza kuwa Wairani watavunja njama za maadui kwa kutekeleza mafundisho ya Qur'ani katika maisha yao ya kila siku. Aidha amepongeza hatua zilizochukuliwa na bunge kueneza mafundisho ya Qur'ani nchini lakini akasema hatua zaidi zinapaswa kuchukuliwa. 737520