IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya Kuwait yatafanywa ya kimataifa

19:00 - January 31, 2011
Habari ID: 2073498
Kamati ya Utendaji ya mashindano ya kitaifa ya kuhifadhi na kusoma Qur'ani Tukufu zawadi ya Kuwait imetoa pendekezo kuwa mashindano hayo yafanyike katika ngazi ya kimataifa.
Gazeti la al Rai linalochapishwa Kuwait limeandika kuwa Mkuu wa Kamati ya Habari ya mashindano hayo Ali al Awadhi amesema pendekezo hilo limetolewa baada ya vikao kadhaa vya mashauriano na taasisi husika wakiwemo maafisa wa Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu.
Amesema maamuzi yaliyochukuliwa yamewasilishwa kwenye kamati ya masuala ya fedha.
Ali al Awadhi ameongeza kuwa katika vikao hivyo kumetolewa mapendekezo mengi ikiwa ni pamoja na kuainisha kipimo cha kiwango cha mafanikio ya mashindano hayo. 739546


captcha