Tovuti ya Khaleej Times imeripoti kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Masuala ya Kiislamu ya Dubai Hamad al Shaibani amesema kuwa sherehe hizo za kuadhimisha Maulidi na kuzaliwa Mtume Muhammad (saw) zitaendelea kwa kipindi cha wiki moja.
Amesema kuwa majlisi za hotuba za wasomi na shakhsia mbalimbali kuhusu maisha na Mtume Muhammad (saw) zitafanyika katika misikiti yote ya Dubai katika kipindi cha wiki nzima.
Mkuu wa kitengo cha ushauri na ulinganiaji wa Jumuiya ya Masuala ya Kiislamu ya Dubai Muhammad al Muhairi pia amesema zaidi ya hotuba 500 kuhusu tabia na maadili ya Mtume Muhammad (saw) zitatolewa na maulamaa na wasomi wa Kiislamu katika kipindi chote cha wiki nzima.
Amesema sira na mwenendo wa Mtume Mtukufu (saw) ambao daima ndiyo kigezo bora kwa ajili ya kutenda wema, kuongoza na kufikia ufanisi hapa duniani na akhera, itajadiliwa katika vikao hivyo. 746865