IQNA

Jamii ya Waislamu wa Ireland yaongezeka

17:56 - February 14, 2011
Habari ID: 2080925
Jamii ya Waislamu wa Ireland imekuwa kwa kiwango kikubwa katika miaka ya hivi karibuni.
Inaripotiwa kuwa jamii ya Waislamu wa Ireland imeongezeka mara 10 zaidi kuliko ilivyokuwa katika kipindi cha miaka 20 iliyopita.
Kituo cha upashaji habari cha Irishcentral kimeripoti kuwa dini ya Kiislamu ndiyo dini inayostawi zaidi kuliko dini nyingine nchini Ireland kutokana na kustawi kwa asilimia 70 idadi ya Waislamu katika miaka ya kati ya 2002 na 2006.
Uchunguzi uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Cork nchini Ireland kuhusu Uislamu nchini humo umeashiria suala la kuwepo Waislamu wa kaumu mbalimbali nchini Ireland na kusema katika nchi nyingi za Ulaya Waislamu huwa ni kutoka kaumu moja tofauti kabisa la Ireland.
Uchunguzi huo umesisitiza kuwa serikali ya Ieland inapaswa kufanya juhudi za kuanzisha uhusiano na misikiti na taasisi za Kiislamu. 747725
captcha