Kwa mujibu wa tovuti ya Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ISESCO, wahubiri, walimu wa shule za Kiislamu na maimamu wa swala za jamaa katika nchi za Ulaya wanashiriki katika warsha hiyo.
Warsha hiyo inafanyika kwa lengo la kuwanufaisha washiriki kuhusiana na mbinu za kisasa za mafunzo, njia za kuimarisha mawasiliano na ujuzi wa mambo mapya katika uwanja wa elimu na utamaduni.
Kuimarisha ushirikiano na mashauriano kati ya maimamu, walimu na wahubiri wa Kiislamu na vilevile kubadilishana uzoefu miongoni mwao ni lengo jingine la kufanyika warsha hiyo. 751661