IQNA

Sheikh Qardhawi atoa fatuwa ya kuuawa Gaddafi

17:13 - February 22, 2011
Habari ID: 2084907
Mwenyekiti wa Muungano wa Maulamaa wa Kiislamu Duniani Sheikh Yusuf Qardhawi ametoa fatwa ya kuuawa dikteta wa Libya Kanali Muammar Gaddafi.
Sheikh Qardhawi ametoa fatuwa hiyo katika mahojiano yake na televisheni ya al Jazeera ya Qatar baada ya ndege za kijeshi za Libya kushambulia wananchi katika mji mkuu wa nchi hiyo Tripoli. Amewataka askari wa jeshi la Libya kuasi amri za Gaddafi akisisitiza kuwa ni haramu kutii mtu anayeamuru kuuawa wananchi. Ameongeza kuwa, mwanajeshi yeyote mwenye uwezo wa kumpiga risasi na kumuua Gaddafi, basi afanye hivyo na kuuondolea umma wa Kiarabu shari ya mwendawazimu huyo mal'uni.
Mwenyekiti wa Muungano wa Maulamaa wa Kiislamu Duniani amesema kuwa amri ya Kanali Gaddafi ya kushambuliwa miji kwa kutumia ndege za kivita ni kielelezo cha kufanya ufisadi katika nchi na kwa msingi huo ni halali kumwaga damu ya dikteta huo. 751953
captcha