Kituo cha habari cha al Youm al Sabi' kimeripoti kuwa, wakati ulimwengu wa Kiarabu unashuhudia wimbi kubwa la mwamko wa mataifa na harakati za kupigania haki zao na huko Libya kunashuhudiwa mauaji ya mamia ya raia wasiokuwa na hatia, Jumuiya ya Uhakiki wa Kiislamu ya al Azhar ilikamilisha kikao chake cha Alkhamisi tarehe 25 Februari bila ya kusema lolote kuhusu masuala hayo.
Jumuiya ya Uhakiki wa Kiislamu ya al Azhar ilitosheka katika kikao hicho kwa kuchunguza suala la utumiaji wa mada za kupoteza fahamu katika kutibu maradhi ya maini na kutayarisha muswada wa adhabu dhidi ya wanaochapisha Qur'ani zenye makosa ya kimaandishi.
Kikao hicho cha Jumuiya ya Uhakiki wa Kiislamu ya al Azhar kimewavunja moyo mno waandishi habari na mashirika ya habari ya ulimwengu wa Kiarabu ambayo yalikuwa yakisubiri taarifa kali ya al Azhar kama taasisi kubwa zaidi ya kidini ya Ahlusunna ya kulaani jinai na mauaji yanayofanywa na Kanali Muammar Gaddafi dhidi ya raia wasiokuwa na hatia nchini Libya.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uhakiki wa Kiislamu ya al Azhar Ali Abdulbaqi alisema kuwa kikao hicho hakukichunguza hali ya mambo katika nchi za Kiarabu na kwamba suala hilo halikuwa katika ajenda yake. 753319