Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu, Sheikh wa al Azhar Ahmad al Tayyib ameutaja utawala wa kidikteta na unaomwaga damu wa Libya kuwa si halali na kwamba ni haramu kwa askari wa nchi hiyo kufuata amri ya kiongozi wake Kanal Muammar Gaddafi.
Taarifa ya Sheikh Amad Tayyib amesema utawala wa Libya umepoteza uhalali wake na ni utawala ghasibu na wa kidhalimu.
Amesema hatua ya Muammar Gaddaf ya kumwaga damu za raia kwa ajili ya kulinda serikali yake na jinai zinazoendelea kufanywa na utawala huo vimeifanya serikali ya Libya kuwa ya kidhalimu. Sheikh wa al Azhar amesema: "Kwa mujibu wa nafasi yangu ya kidini, kitaifa na kibinadamu ninawataka maafisa wa serikali, maafisa wa jeshi na askari wasifuate amri za utawala wa kidikteta na unaomwaga damu za wananchi wasiokuwa na hatia wa Libya."
Sheikh wa al Azhar amewataka pia Waarabu na Waislamu wote, wapenda uhuru na mataifa yote duniani kuwatumia misaada ya kibinadamu na kitiba wananchi wa Libya. 754406