Kufuatia malalamiko na maandamano yanayofanywa na Waislamu wa madhehebu ya Shia katika maeneo yenye Waislamu wengi wa mdhehebu ya Shia nchini Saudi Arabia, serikali ya Riyadh imeamua kupunguza mbinyo dhidi ya shughuli za kidini za Mashia na kufungua baadhi ya misikiti ya wafuasi wa madhehebu hiyo.
Kanali ya habari ya Rasid imetangaza kuwa baada ya kushadidi maandamano na mwamko wa Kiislamu Mashariki ya Kati na Saudi Arabia, serikali ya Riyadh imechukua uamuzi wa kufungua baadhi ya misikiti ya Waislamu wa madhehebu ya Shia iliyofungwa tangu mwaka 2008 katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo la al Khubar.
Mashia wa mji huo wanataka misikiti yao yote iloyofungwa na serikali ifunguliwe. Inasemekana pia kuwa serikali ya Saudia imefungua pia misikiti ya Waislamu wa madhehebu ya Shia katika miji ya Abqi, Raas Tannura na al Jubail.
Waislamu wa madhehebu ya Shia wa mji wa al Khubar nchini Sadia wamekuwa wakitekeleza swala za jamaa barabarani baada ya serikali kufunga misikiti yao mwaka 2008 na kuwatia nguvuni shakhsia na wasomi kadhaa wa madhehebu hiyo. 755480