IQNA

Hatibu wa swala ya Ijumaa wa Ihsaa Saudi Arabia akamatwa

14:52 - March 01, 2011
Habari ID: 2088641
Askari usalama wa Saudi Arabia siku ya Jumapili tarehe 27 Februari walimtia nguvuni Hujjatul Islam wal Muslimeen Taufiq al-Amir hatibu wa Ijumaa wa mji wenye wakazi wengi wa Kishia wa Ihsaa nchini Saudi Arabia.
Kwa mujibu wa tovuti ya Raswid, Taufiq al-Amir ni mmoja wa wanazuoni mashuhuri wa Kishia wa Saudi Arabia ambaye amekuwa akitetea kwa uwezo wake wote haki za Waislamu wa madhehebu ya Shia na uhuru wa kiraia katika nchi hiyo.
Al-Amir alitiwa nguvui hivi karibuni na askari usalama baada ya kutaka marekebisho ya kimsingi ya kikatiba yafanyike katika ufalme wa nchi hiyo. Alitiwa nguvuni mara tu baada ya kuripoti kwenye kituo cha polisi cha mji wa Damman kama alivyotakiwa kufanya na polisi ya mji huo.
Katika hotuba za swala ya Ijumaa iliyopita al-Amir aliwataka watawala wa Saudi Arabia kufanya marekebisho ya kimsingi ya kisiasa nchini humo, kuondoa ubaguzi wa kimadhehebu na kuufanya mfumo wao wa kifalme kuwa wa kikatiba.
Hujjatul Islam al-Amir ametiwa nguvuni mara nyingi na askari usalama wa Saudia kwa kutaka watawala wa nchi hiyo waruhusu kufanyika kwa uhuru shughuli za kimadhehebu za Waislamu wa Kishia. 755383
captcha