IQNA

Kamati ya Kimataifa ya Mshikamano yawasili Gaza

22:11 - March 08, 2011
Habari ID: 2092744
Ujumbe wa Muungano wa Kimataifa wa Kukomesha Mzingiro wa Wazayuni huko Gaza umeingia katika eneo hilo kupitia kivuko cha Rafah.
Kituo cha habari cha Palestine Info kimeripoti kuwa hii ni mara ya kwanza kwa ujumbe huo unaojumuisha wawakilishi wa nchi mbalimbali kuingia katika Ukanda wa Gaza kupitia kivuko ch Rafah baada mapinduzi ya wananchi Misri.
Ujumbe huo umepitisha pia mfuko mmoja wa simenti katika kivuko hicho kama ishara ya kuanza kujenga upya Ukanda wa Gaza ulioharibiwa vibaya na mashambulizi ya utawala ghasibu wa Israel.
Ujumbe huo umepokewa na kamati ya serikali ya kuvunja mzingiro wa Gaza.
Msemaji wa kamati hiyo Amad al Asi amesema ujumbe huo unawashirikisha wawakilishi wawili wa Misri, wawili kutoka Ireland, wawili kutoka Uingereza, wawili kutoka Marekani, mmoja kutoka Poland na wawakilishi wawili kutoka Ugiriki.
Amesema wawakilishi wa Misri katika kamati hiyo ni wanaharakati walioshiriki katika mapinduzi yaliyong'oa madarakani serikali ya kiongozi wa zamani wa nchi hiyo Hosni Mubarak. 760348
captcha