Kwa mujibu wa tovuti ya jumuiya hiyo, kikao hicho kilifanyika kwa ombi la Ekmeleddin Ihsanoglu, Katibu Mkuu wa OIC kwa madhumuni ya kuchunguza hali ya wakimbizi wa Libya ambao wanakimbia maeneo ya vita kati ya wanamapinduzi na magenge ya mauaji yanayotumiwa na Dikteta Muammar Gaddafi kwa lengo la kuzima mapinduzi hayo.
Ihsanoglu amezitaka nchi wanachama wa OIC pamoja na mashirika ya kimataifa kuwasaidia raia waathirika wa ghasia hizo ambazo zimekuwa zikiendelea kwa wiki kadhaa sasa kwa madhara ya raia wa kawaida wasio na ulinzi.
Siku chache zilizopita pia Katibu Mkuu huyo alishirikiana na Ban Ki Moon Katibu Mkuu mwenzake wa Umoja wa Mataifa na wawakilishi wa mashirika mengine ya kimataifa kupitia mazungumzo ya video, kuchunguza njia za kuwafikishia misaada ya kibinadamu waathirika wa machafuko hayo. 758955