Akizungumza na kanali ya televisheni ya Serbia, Bw. Nozariyan amesema mwamko wa Kiislamu katika eneo la Mashariki ya Kati umetokana na juhudi za wanawake na wanaume."Kwa mtazamo wa Kiislamu, nafasi ya mwanamke katika nyanja zote za kiutamaduni, kijamii na kisiasa ni muhimu kwa sababu Uislamu unampa mwanaume na mwanamke haki sawa".
Nozariyan amengoeza kuwa nchini Iran wanawake wana nafasi kubwa katika sekta za utamaduni na elimu. "Zaidi ya asilimia 65 ya wanafunzi wa vyuo vikuu ni wasichana na wanawake. Wanawake Waislamu wa Iran pia wamepata mafanikio makubwa katika mashindano ya kimataifa ya michezo na sanaa", amesema msomi huyo.
Ameongeza kuwa wanawake wa Iran pia wanashikilia nyadhifa muhimu serikalini kama makamu wa rais, waziri na vilevile nafasi katika bunge. "Wanawake wa Iran wameheshimu amri ya Mwenyezi Mungu kuhusu vazi la hijabu huku wakishiriki katika kazi mbalimbali", amesema.
760811