IQNA

Ujumbe wa ISESCO katika Siku ya Kimataifa ya Wanawake

17:57 - March 10, 2011
Habari ID: 2093520
Shirika la Kiislamu la Elimu, Sayansi na Utamaduni ISESCO limetoa wito wa kuandaliwa mazingira yanayofa kwa ajili ya uwezeshaji wanawake katika ulimwengu wa Kiislami ili wawe na nafasi katika ustawi endelevu.
Katika taarifa kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Wanawake iliyoadhimishwa Jumatano tarehe 9 Machi, ISESCO imesisitiza haja ya mazingira kuandaliwa ili kuwakomboa wanawake kutoka minyororo ya ujinga na maendeleo duni mambo ambayo yanakinzana na sheria za Kiislamu ambazo zinasisitiza kuhusu haki za mwanaadamu bila kuwepo ubaguzi za kijinsia.
Taarifa hiyo ya ISESCO imesema maendeleo ya wanawake na kuhusishwa kwao katika shughuli za umma pamoja na kustawisha maisha yao kwa ajili ya maendeleo ya kijanii ni wajibu wa kidini. ISESCO imesema nchi za Kiislamu zinapaswa kuimarisha elimu ya wanawake na kuwawezesha wanawake Waislamu wawe na nafasi katika ubunifu wa kisayansi. Taarifa hiyo imesema uwezeshaji wanawake Waislamu katika masuala ya sayansi na teknolojia ni muhimu katika mradi ya kistaarabu wa Ulimwengu wa Kiislamu.
760920
captcha