IQNA

Kikao cha 'Kuirekebisha Jamii' kufanyika India

15:05 - April 11, 2011
Habari ID: 2104152
Kikao chenye anuani ya 'Kuirekebisha Jamii' maalumu kwa wanawake kitafanyika Aprili 16-17 chiani ya usimamizi wa Bodi ya Waislamu ya Kitaifa ya Sheria Binafsi mjini New Delhi.
Siku ya kwanza ya kikao hicho washiriki watajadili 'haki za wanawake na majukumu yao'. Siku ya pili maulamaa mashuhuri wa India kama vile Sheikh Mohammad Mukkharam Ahmad, Imamu wa Msikiti wa Jamia wa Fatahpuri watahutubu.
Wanaharakati wanawake Waislamu nchini India pia wanatazamiwa kuhutubu katika kikao hicho.
Idadi ya Waislamu nchini India inakadiriwa kuwa milioni 150 kati ya watu bilioni 1.2.
771469
captcha