IQNA

Maombolezo ya shahada ya Bibi Fatma (as) kufanyika mjini London

11:42 - April 18, 2011
Habari ID: 2107627
Maombolezo ya kukumbuka kuawa shihidi Bibi Fatma (as) binti ya Mtukufu Mtume (saw) yamepangwa kufanyika Mei 5 katika Kituo cha Kiislamu cha London Uingereza.
Kwa mujibu wa tovuti ya ic-el, maombolezo hayo ambayo yameandaliwa na kituo kilichotajwa yatahudhuriwa na wakuu wa taasisi na mashirika mbalimbali ya Kiislamu ya Uingereza pamoja na wafuasi wa madhehebu ya Watu wa Nyumba ya Mtume, Ahlul Beit (as). Maombolezo hayo yataendelea kwa muda wa siku tano ambapo wanazuoni na wanafikra mbalimbali wa Kiislamu watazungumzia fadhila na maisha ya mtukufu huyo wa Kiislamu. Maombolezo hayo yatakuwa yakifanyika kila usiku mara tu baada ya kuswaliwa swala za Maghrib na Ishaa kuanzia saa 3 usiku kwa wakati wa Uingereza. 776134
captcha