IQNA

Msikiti mkubwa kujengwa nchini Ufaransa

12:02 - April 19, 2011
Habari ID: 2108307
Msikiti mkubwa ulio na uwezo wa kubeba watu wapatao 3000 unatarajiwa kujengwa hivi karibuni katika mji wa Charleville-Mézières nchini Ufaransa.
Kwa mujibu wa tovuti ya lunion.presse msikiti huo utakaojengwa kwa udhamini wa Jumuiya ya Misikiti na Vituo vya Kidini na Kiutamaduni ya Ufaransa Ardennes unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka ujao wa 2012. Kituo cha utamaduni na masuala ya Kiislamu, ukumbi wa mikutano ya kidini na vilevile clasi za masomo ya Qur'ani zitajengwa pambizoni mwa msikiti huo. Ujenzi wa msikiti unatazamiwa kuanza mapema mwezi ujao wa Mei. Meya wa mji uliotajwa hatimaye alikubali ombi la Waislamu la kujengwa msikiti katika mji huo baada ya uafuatiliaji wa miaka mingi. 776464
captcha