Kwa mnasaba huo, maduka na masoko yote ya mji huo yamefungwa na bendera nyeusi kupeperushwa kwenye nyumba na majengo ya mji huo kama alama ya maombolezo ya Waislamu kumpoteza mtukufu huyo wa Watu wa Nyumba ya Mtume (saw). Idara inayosimamia haram mbili za Imam Hussein na Abul Fadhl Abbas (as) ambako ndiko kunakofanyika maombolezo hayo, imesema kuwa mambo yote yamekwishaandaliwa kwa ajili ya kuwahudumia kwa njia bora waombolezaji na wafanyaziara katika sehemu hiyo takatifu. Idara hiyo imesema kwa kuhuishwa maombolezo hayo, waombolezaji wanajaribu kuwafikishia walimwengu mafundisho ya Ahlul Beit (as) pamoja na mateso na dhulma kubwa waliyofanyiwa na watawala dhalimu wa zama zao. 776515