Kwa mujibu wa tovuti ya 20minutes askari usalama hao walimtia nguvuni mwandishi huyo baada ya kuvamia sehemu anayofanyia kazi hapo siku ya Jumapili. Jumuiya ya kutetea haki za binadamu ya Human Rights First Society imethibitisha habari hiyo na kuongeza kuwa askari hao walichukua vyombo na vifaa anavyofanyia kazi mwandishi huyo ikiwemo kompyuta yake binafsi. Mafisa wa Saudia hawajatoa maelezo yoyote kuhusiana na sababu za kukamatwa mwandishi huyo wa Kishia. Utiwaji nguvuni wa mwandishi huyo unafanyika katika hali ambayo ufalme wa Saudia katika siku za hivi karibuni umezidisha vitendo na hatua zake za kuwakandamiza na kuwatia nguvuni kiholelewa wanaharakati wa Kishia wanaoishi katika miji ya mashariki mwa nchi hiyo. Katika upande wa pili wakazi wa maeneo hayo wamekuwa wakifanya maandamano ya kulalamikia jambo hilo na kuutaka utawala wa nchi hiyo uwaachilie mara moja wafungwa wa kisiasa ambao wanashikiliwa na utawala huo bila kufikishwa mahakamani. 777718