IQNA

kamil Kabtan:

Shughuli za msikiti wa Lyon zinafahamika vyema

17:11 - April 30, 2011
Habari ID: 2113589
Mkurugenzi wa Msikiti Mkuu wa Lyon Kamil Kabtan amekanusha vikali madai ya viongozi wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani yaliyofichuliwa na mtandao wa Wikileaks kwamba eneo hilo la Kiislamu linatumiwa kwa ajili ya shughuli za kigaidi.
Taarifa iliyotolewa Kamil Kabtan imezitaja tuhuma hizo za maafisa wa serikali ya Marekani kuwa ni maskhara na kuongeza kuwa msikiti na Kituo cha Kiislamu cha Lyon ambacho ni taasisi inayopigiwa mfano kinafahamika kwa watu wote na tuhuma zisizokuwa na msingi kama hizo haziwezi kushusha hadhi ya kituo hicho cha Kiislamu.
Katika sehemu nyingine ya taarifa yake Kamil Kabtan amesema anatarajia kukutana uso kwa uso na balozi wa Marekani nchini Ufaransa na kuwasilisha malalamiko na masikitiko yake kuhusu madai hayo yasiyokuwa na msingi wowote.
Mtandao wa Wikileaks umechapisha kwamba viongozi wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani wanakituhumu Kituo cha Kiislamu na Msikiti Mkuu wa Lyon kuwa ni kituo cha kueneza ugaidi barani Ulaya! 782124


captcha