Japokuwa habari ya kuuawa Bin Laden bado inazua maswali mengi katika jamii ya kimataifa huku wengi wakisema kuwa inatumiwa na Rais Barack Obama kwa malengo ya kisiasa, lakini Sheikh Mkuu wa al Azhar amesema baada ya kusikia kwamba maiti ya Usama bin Laden imetupwa bahari kwamba, hatua hiyo haifai.
Amesema kutupa mwili wa maiti baharini kunapingana na thamani za Kiislamu na kibinadamu. Ameongeza kuwa sheria za dini ya Kiislamu zinakataza kuharibu na kuvunjia heshima mwili wa maiti bila ya kujali dini wala kaumu yake na zinawalazimisha watu kuheshimu maiti wakati wa kuzika.
Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Nabil al Arabi amesema Cairo inapinga utumiaji mabavu wa aina yoyote hata ule unaofanyika katika nyanja za kimataifa na kwamba serikali ya Misri haina mtazamo wowote kuhusu mauaji ya Usama bin Laden.
Maafisa wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani wametangaza kuwa mwili wa kiongozi wa al Qaida Usama bin Laden umetupwa baharini kwa kisingizio kwamba kaburi lake lisije likatembelewa na watu. 785889