IQNA

Wafaransa kukumbuka Siku ya Maafa Palestina

22:36 - May 14, 2011
Habari ID: 2121996
Wananchi wa Ufaransa wamepanga kufanya maandamano katika miji mbalimbali ya nchi hiyo sambambaa na kuwadia tarehe 15 Mei ambayo inajulikana kwa wananchi wa Palestina kama Siku ya Nakba au Siku ya Maafa ambayo inakumbusha tukio la kuvamiwa na kukaliwa kwa mabavu ardhi ya Palestina.
Ripoti zinasema kuwa jumuiya zinazowaunga mkono Wapalestina hususan kundi la Mshikamano na Mapambano katika Ulimwengu wa Kiarabu, yametoa taarifa mbalimbali yakiwataka Waislamu na wasiokuwa Waislamu kuandamana siku ya tarehe 15 Mei katika miji mbalimbali kwa ajili ya kupinga uvamizi wa Wazayuni dhidi ya ardhi ya Palestina.
Taarifa ya kundi la Mshikamano na Mapambano ya Ulimwengu wa Kiarabu imesema kuwa tarehe 15 Mei mwaka huu inapaswa kupewa jina la Siku yaa Palestina katika harakati za mapambano ya ulimwengu wa Kiarabu na walimwengu wote wanapaswa kukwamisha malengo ya utawala ghasibu wa Israel.
Taarifa hiyo imesema kuwa wananchi wa Paris watakutana saa tisa jioni katika Medani ya Jamhuri kwa ajili ya kuwaunga mkono na kuwatetea wananchi wanaokandamizwa wa Palestina.
Baadhi ya wakimbizi wa Kipalestina watasimulia masaibu yaliyowapata kutoka kwa askari wa utawala ghasibu wa Israel. 790867

captcha