IQNA

WHO:

Serikali ya Bahrain inalazimika kuonyesha ukweli wa mambo

19:21 - May 16, 2011
Habari ID: 2123331
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ameitaka serikali ya Bahrain kutoa taarifa kamili ya matukio yanayojiri nchini humo kwa jumuiya za kimataifa na vyombo vya habari.
Margaret Chan aliyasema hayo katika mazungumzo yake na Waziri wa Maendeleo ya Jamii ambaye pia anasimamia Wizara ya Afya ya Bahrain Fatima Blushi.
Bi. Chan amesema serikali ya Manama inapaswa kutoa ripoti na habari zaidi kuhusu hali ya ndani ya nchi hiyo na kudhihirisha ukweli wa mambo kwa jumuiya za kimataifa na vyombo vya mawasiliano ya umma. Mkurugenzi Mkuu wa WHO pia ameitaka serikali ya Bahrain kutayarisha mazingira mazuri ya huduma za afya kwa raia wote wa nchi hiyo.
Madaktari na wauguzi wengi wa Bahrain wametiwa nguvuni na jeshi la nchi hiyo kwa kosa la kutoa huduma za matibabu kwa vijana wanaojeruhiwa katika maandamano ya amani ya kutaka marekebisho. 792992
captcha