IQNA

Kiongozi wa Mashia wa Bahrain:

Harakati ya wananchi ni kwa ajili ya mageuzi

10:36 - May 22, 2011
Habari ID: 2126205
Kiongozi wa Waislamu wa Kishia wa Bahrain Ayatullah Issa Qasim amesema kuwa harakati ya mapambano ya wananchi dhidi ya utawala wa Manama ni ya amani ya watu wanaotaka marekebisho.
Ayatullah Issa Qasim amesema kunyamaza kimya kwa mataifa mbalimbali dhidi ya watawala dhalimu katika zama hizi kutasababisha mlipuko na machafuko makubwa katika siku za usoni.
Ameongeza kuwa licha ya matakwa ya wananchi wa Bahrain yanayoshuhudiwa kila siku na walimwengu wote lakini watawala wa kifalme wa Manama hawajabadilika na kwamba harakati hiyo ya wananchi ya kutaka marekebisho ya kisiasa na kijamii itaendelea.
Kiongozi wa Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Bahrain amesisitiza kuwa uungaji mkono wa baadhi ya nchi kwa dhulma na ukandamizaji unaofanwa na serikali ya Bahrain kwa ajili ya kulinda maslahi yao hautafanikiwa mbele ya irada na azma ya wananchi. 795391

captcha