Taarifa hiyo kali ya wabunge wa Bulgaria imekemea na kulaani mashambulizi yaliyofanywa na wafuasi wa chama cha Ataka dhidi ya Waislamu waliokuwa wakitekeleza ibada katika msikiti huo.
Taarifa hiyo imesema shambulizi hilo ambalo limefanyika dhidi ya Waislamu waliokuwa wakitekeleza ibada siku ya Ijumaa ni hatua ya kuaibisha ambayo haiwezi kufumbiwa macho.
Sehemu nyingine ya taarifa ya bunge la Bulgaria imesema kitendo hicho kitatayarisha mazingira ya kutokea mivutano na ghasia za kidini na imetahadharisha juu ya matokeo yake mabaya.
Shambulizi la wafuasi wenye misimamo mikali wa chama cha Ataka dhidi ya msikiti wa Banya Bashi limesababisha mgawanyiko ndani ya chama hicho chenyewe na kuwafanya baadhi ya wawakilishi wake bunge kujitenga. 799317