Taasisi hiyo iliyoanzishwa kwa mnasaba wa sherehe za kuadhimisha kuzaliwa Bibi Fatima Zahra SA itakuwa na jukumu la kutoa misaada kwa mayatima na huduma nyinginezo katika jamii. Sherehe hizo zilifanyika 24 Mei mjini Zaria katika jimbo la Kaduna kaskazini mwa Nigeria na kuhudhuriwa na maelfu ya Waislamu hasa wafuasi wa madhehebu ya Shia.
Katika hotuba yake Sheikh Zakzaki alitoa wito kwa Waislamu kuishi maisha ya kifamilia kwa mujibu wa sheria za Kiislamu. Sheikh Zakzaki alifafanua kuhusu nafasi ya Bibi Fatima Zahra SA ambapo aliashiria hadithi za Mtume SAW kuhusu Bibi Fatima SA kwa mujibu wa hadithi za Kisuni na Kishia. Alizungumzia kuhusu haki za wanawake katika jamii ya leo na kukosoa vikali watu ambao wanawanyima wanawake Waislamu haki zao.
Katika hafla hiyo, Sheikh Zakzaki alitoa zawadi kwa wanafunzi waliofaulu katika mashindano kuhusu maisha ya Bibi Fatima Zahra.
Akizungumza katika sherehe hizo, mwanaharakati wa Kiislamu Bi. Malama Zeenah Ibrahim alifafanua kuhusu maisha ya bibi Fatima Zahra SA.
Aidha katika sherehe hizo kulizinduliwa DVD ya Maisha ya Mapambano ya Imam Khomeini RA iliyofasiriwa kwa lugha ya Kihausa.