IQNA

Meli ya misaada ya kibinadamu kutoka Ufaransa kuelekea Gaza

19:02 - June 08, 2011
Habari ID: 2135157
Meli inayobeba misaada ya kibinadamu kwa ajili ya raia wanaozingirwa na utawala haramu wa Israel wa Ukanda wa Gaza inatazamiwa kuelekea Palestina tarehe 18 Juni ikitokea Bandari ya Marseille.
Meli hiyo ilipangwa kuelekea Gaza mwanzoni mwa mwezi huu wa Mei lakini safari hiyo imecheleweshwa kutokana na matatizo ya kisiasa.
Meli hiyo itakuwa na makumi ya wanachama wa jumuiya za kiraia, waandishi habari na shakhsia mbalimbali wa Kifaransa. Meli nyingine kama hiyo zenye misaada ya kibindanu kutoka Uturuki na Ugiriki zinajiunga na meli hiyo ya Ufaransa kuelekea Gaza kwa ajili ya kuvunja mzingiro wa wazayuni dhidi ya raia milioni moja na nusu wanaosumbuliwa na uhaba mkubwa wa bidhaa muhimu kama chakula, maji na dawa. 805241



captcha