Katika mazungumzo yake na ujmbe wa Taasisi ya Uenezi ya Mapinduzi ya Februari 17 nchini Libya, Ahmad al Tayyib amesema mataji na viti vya ufalme vya serikali za Kiarabu havina thamani ya kumwaga damu ya raia.
Ameelezea wasiwasi wake kuhusu yanayojiri katika nchi za Kiarabu na amewataka viongozi wa nchi hizo kujibu wema na upendo wa mataifa yao ambayo yamestahamili dhulma na ufisadi wao kwa kipindi cha miaka mingi kwa kujiengua madarakani.
Sheikh wa al Zahrar amesema iwapo kubakia madarakani kutapelekea kumwagika damu za raia, basi viongozi wa nchi za Kiarabu wanalazimika kuondoka madarakani haraka iwezekanavyo.
Amesema kuwa al Azhar inaunga mkono kwa dhati mapinduzi ya wananchi wa Libya, Yemen na nchi nyingine za Kiarabu na kwamba taasisi hiyo ya kidini itaendelea kusimama bega kwa bega na wananchi wa Libya. 809478