Samiir Dailo ambaye ni mwanachama wa Bodi ya Utendaji ya harakati ya al Nahdha amesema kuwa wananchi wote wa Tunisia wanapinga suala la kuwepo uhusiano kati ya nchi yao na utawala ghasibu wa Israel.
Hatua hiyo mechukuliwa baada ya kikao cha Baraza Kuu la Utekelezaji wa malengo ya mapinduzi ya Tunisia kilichofanyika mjini Tunis. Baadhi ya wajumbe walioshiriki katika kikao hicho wametoa wito wa kurejeshwa uhusiano wa kawaida na utawala ghasibu wa Israel.
Dailo amesema kuna baadhi ya watu waliopenya na kuingia katika taasisi mbalimbali ambao wanatoa mitazamo ya kuaibisha na inayokwenda kinyume na nafasi na heshima ya Watunisia.
Vilevile Ahmad al Kahlawi, mjumbe wa kituo cha taifa cha kuunga mkono mapambano ya wananchi amesema kurejeshwa uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel kunapingana na malengo ya mapinduzi ya wananchi wa Tunisia.
Dikteta wa zamani wa Tunisia Bin Ali aling'olewa madarakani mapema mwaka huu kufuatia wimbi kubwa la mapinduzi ya wananchi. 810585