IQNA

Kikao cha Muungano wa Redio za Kiislamu chafanyika Jeddah

17:14 - June 20, 2011
Habari ID: 2141412
Kikao cha dharura cha Muungano wa Redio za Kiislamu kilifanyika jana Jumapili kwenye makao makuu ya muungano huo katika mji wa Jeddah nchini Saudi Arabia.
Akizungumza kwenye kikao hicho Abdul Aziz Khojah, Waziri wa Utamaduni na Upashaji Habari wa Saudia umesema kuwa ulimwengu hivi sasa unashuhudia mlipuko mkubwa usiotarajiwa wa bahari ambao una athari kubwa katika nyanja za kisiasa, kitamaduni, kijamii na kiuchumi. Ametaka nchi za Kiislamu kunufaika na teknolojia ya kisasa kwa ajili ya kuhudumia vyema dini na masuala ya Kiislamu duniani.
Kikao cha Jeddah kimefanyika kwa ajili ya kupasisha muundo mpya wa muungano huo na kujadiliwa suala la ugombeaji wa mkurugenzi mkuu wa baadaye wa muungano huo kwa msingi wa mgawanyo wa kijiografia wa nchi za Kiislamu. Mkurugenzi Mkuu wa hivi sasa wa muungano huo ni raia wa Malaysia ambaye anatarajiwa kujiuzulu mwezi Novemba mwaka huu na kuwacha wazi nafasi hiyo kwa ajili ya kuchukukiwa na mkurugenzi mkuu mpya.
Muungano huo wa idhaa za Kiislamu ulibuniwa mwaka 1975. 811819
captcha