Mwanafikra wa Saudi Arabia ambaye pia ni Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Kistratijia katika masuala ya Ghuba ya Uajemi Ali al Ahmadi amesema kuwa viongozi wa utawala wa Aal Khalifa nchini Bahrain na Aal Saud wa Saudia wanatumia mamluki wa Kiasia kwa ajili ya kukandamiza wananchi anaoandamana kupinga serikali ya Bahrain.
Ali al Ahmadi amesema viongozi wa serikali ya Bahrain wanawatumia mamluki kutoka Indonesia, Pakistan na Malaysia kwa ajili ya kuzima na kukandamiza harakati ya mageuzi ya wananchi.
Ameongeza kuwa viongozi wa utawala wa Aal Khalifa hawana imani tena na hata jeshi la watu wao wa karibu, suala ambalo limewafanya wawatumie mamluki wa kigeni.
Mwanafikra huyo wa Saudia amesema viongozi wa utawala wa kifalme wa Bahrain wanahofia kwamba vibaraka wao wa ndani yumkini wakaungana na wananchi na kwa msingi huo wameamua kuajiri mamluki kutoka nchi za kigeni.
Wakati huo huo Saudi Arabia imeziomba serikali za Malaysia na Pakistan kutuma maafisa wa usalama nchi Bahrain kwa shabaha ya kulinda mamluki wanaotumiwa kukandamiza harakati za wananchi. 812573