IQNA

Al Azhar yataka kuasisiwa serikali isiyokuwa ya kidini Misri!

15:32 - June 21, 2011
Habari ID: 2142097
Sheikh wa al Azhar nchini Misri Ahmad Tayyib ametoa wito wa kuasisiwa serikali isiyokuwa ya kidini nchini humo!
Shirika la habari la Ufaransa (AFP) limemnukuu Sheikh wa al Azhar akitoa maelezo kuhusu uhusiano wa dini na serikali nchini Misri.
Ameashiria matokeo ya mazungumzo ya maulamaa wa al Azhar kuhusu uhusiano kati ya dini na serikali baada ya kung'olewa madarakani utawala wa Hosni Mubarak na akaongeza kuwa maulamaa wote wa al Azhar wanakubaliana juu ya kuundwa serikali ya kitaifa na kidemokrasia itakayojali haki za wananchi wote.
Sheikh Tayyib amesema hati iliyotiwa saini na maulamaa wa al Azhar inasisitiza kuwa dini ya Kiislamu ndio marejeo na chanzo kikuu cha sheria zilizopo katika katiba na jamii lakini dini na serikali vinapaswa kutenganishwa.
Sheikh wa al Azhar ameongeza kuwa hati hiyo pia imezungumzia suala la wafuasi wa dini mbalimbali na kwamba serikali inawajibika kulinda maeneo ya ibada ya dini za mbinguni na imetambua aina zote za ubaguzi na mashambulizi dhidi ya wafuasi wa dini za mbinguni kuwa ni jinai dhidi ya taifa la Misri. 812601

captcha